Mtakatifu Fransisko wa Asizi

Mtakatifu Fransisko wa Asizi (1182-1226), sherehe 4 oktobri
“Ewe Baba, Bwana wa mbingu na dunia, nakutukuza, kwa sababu umewafumbulia waliowadogo mafumbo ya ufalme” (Mt 11, 25).
Fransisko wa Asizi ni mmoja wa wale wadogo waliopokea ufunuo wa mafumbo ya ufalme. Kijana Fransisko pa umri wa myaka 20 alichungua hali ya inchi yake, akasali na kusikiliza neno la Mungu kwenye ibada ya misa. Ndipo akatambua sauti ya Mungu mbele ya msalaba pale kanisa ya Mtakatifu Damiano: “Fransisko uwende ukatengeneze kanisa langu linalobomoko”. Polepole Fransisko akaacha tamaa ya feza na ya cheo cha mfanya vita na kuelekea mambo ya kuongoka moyoni na kusaidia maskini na wagonjwa wa ukoma.
Myaka michache kabla ya kuanga dunia hii, Fransisko wa Asizi, pa umri wa myaka 44, akachunguza maishani mwake na akatambua kama ni neema ya Mungu ilimwezesha kuishi maisha mapya. Katika testament yake akandika hivi:
“Tazama namna gani Bwana amenipatia, mimi ndugu Fransisko, neema ya kuanza kubadilisha mwenendo na kufanya kitubio. Wakati nilikuwa katika zambi, ilikuwa vigumu kwangu kuangalia mtu mwenye ukoma. Lakini Bwana mwenyewe akanipeleka kati yao; nikawatunza na moyo wangu wote; na kiisha yake, yaliyokuwa uchungu kwangu ikageuka ya kupendeza kwa roho na kwa mwili. Nikangoja kidogo, na badaye nikaacha mambo ya dunia.
Pia Mungu akanipa imani kubwa katika makanisa. Ndipo nikatunga sala hii: ‘tunakuabudu, ewe Yesu Kristo, hapa na katika kanisa zote za dunia nzima, na tunakusifu kwa maana umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu’. Tena Bwana akanipa na anaendelea kunipa leo imani kubwa katika mapadri wanaofwata kanuni ya Eklezia ya Roma… sitaki kutambua ndani mwao zambi, lakini Mwana wa Mungu wanaotuletea katika utumishi wao wa kikohani wanapofanya ibada ya ukaristia, wakitulisha kwa mwili na damu ya Bwana wetu Yesu Kristo… Wafundisha dini wote, na wote wenye kazi ya kutangaza neno la Mungu, tunapashwa kuwaheshimu kwa sababu wanatuletea Roho na Uzima.
Kiisha kunipatia Wandugu (mafrera), Bwana mweyewe akaniongoza katika njia ya Enjili, nikaandika kanuni na Papa wa Roma akaikamilisha na kuiitika. Tukajifunza kuishi katika umaskini. Tulikuwa watu wanyonge, tulikuwa tukitumika kwa mikono yetu na ninaomba asiyejuwa ufundi ajifunze na kutumika ili akule tunda la kazi yake na zaidi ili afukuze vishawishi vinavyozunguka kila mtu mvivu na mtu mkosa kazi. Kwa kusalimu watu, tulikuwa tukisema: ‘Bwana awape amani’”.

Ndugu wapenzi, katika andiko hili la Fransisko wa Asizi tunapata mafundisho mengi:
1. Kutambua neema ya Mungu katika hadisi ya maisha yetu. Kutambua Kristu katika maskini wanaotujia. Fransisko alianza kuongoka bila kukaza wengine, ila aliwavuta kwa mfano wake.
2. Imani na heshima kwa kanisa, maana nyumba na mkutano wa wakristu.
3. Sala na heshima kwa msalaba wa Yesu. Tukumbuke kama siku moja Fransisko alisali hivi: “Baba, unipe nisikie moyoni mwangu mapendo iliyompeleka Mwana wako msalabani na nisikie mateso yake mwilini mwangu”. Ndipo Fransisko akachapwa vidonda vitano vya Yesu katika mwili wake. Ndiye mtu wa kwanza aliyepokea alama hiyo yakushuhudia kama alimkaribiya Yesu Kristo kwa maisha yake.
4. Imani na heshima kwa mapadri, kutambua ukubwa wa kazi yao ya kufanya ukaristia, alama ya ujio wa Kristo kati yetu.
5. Kupokea na roho ya kindugu wengine waliotafuta njia ya kuongoka moyoni na kugeuza mwenendo. Ndipo wakazindua pamoja shirika mpya katika Eklezia, inayoitwa: Ordres des Frères Mineurs maana SHIRIKA LA NDUGU WANYONGE. Ni watu wenye kushirikiana na watu wanyonge wa wakati wao, wakiisha kindugu na watu wa kila dini na kila kabila.
6. Heshima kwa wakubwa wa Eklezia ya Roma iliotoka kwa Mitume. Fransisko alitambua neema ya Mungu katika kukubaliwa kanuni na Papa, maana kupewa ruhusa ya Papa kuishi kanuni Fransisko aliotunga.

Tukikumbuka siku za wakati wa Fransisko, katika Eklezia kulikuwa magumu na vikwazo sawa leo, lakini Fransisko ni sawa mama mwenyekusafisha mtoto. Kuna njia mbili yakusafisha mtoto: a. Wengi leo wanafanya sawa mama mmoja aliesafisha mtoto, akaona uchafu na akasahau kama mtoto yumo majini ya uchafu. Ndipo akatupa maji ya uchafu pamoja na mtoto…. b. Mwengine mama, sawa Fransisko, akasafisha mtoto, akatupa maji ya uchafu na akalinda mtoto. Ndiyo maana ya ile aliko la Yesu kwa Fransisko mbele ya msalaba kanisani mwa Mtakatifu Damiano: “Fransisko uwende ukatengeneze kanisa langu…” Kila mmoja wetu anapewa ile ile ujumbe: “uwende ukatengeneze kanisa langu…”
Fr Pierre Matabaro Chubaka, ofm

Une réflexion au sujet de « Mtakatifu Fransisko wa Asizi »

Votre commentaire

Entrez vos coordonnées ci-dessous ou cliquez sur une icône pour vous connecter:

Logo WordPress.com

Vous commentez à l’aide de votre compte WordPress.com. Déconnexion /  Changer )

Image Twitter

Vous commentez à l’aide de votre compte Twitter. Déconnexion /  Changer )

Photo Facebook

Vous commentez à l’aide de votre compte Facebook. Déconnexion /  Changer )

Connexion à %s